HABARI ZA KIGAMBONI







Soko kuu  la uuzaji na ununuaji samaki Ferry likiwa limesaidia kuinua vipato na kuwapatia watu ajira.Hii ni moja ya mafanikio kwani shughuli hizi sasa zinafanywa katika mazingira yanayofaa hivyo kupunguza uharibifu wa mazingira na uharifu.Hivyo serikali haina budi kuboresha swala usafi na mazingira kwa ujumla ili kuhakikisha soko hili linakuwa la manufaa na faida kwa jamii ya wakazi ndani na nje ya kigamboni,hata ikiwezekana lijengwe tena la nyongeza kwa ajili ya wakazi wa Kigamboni ambao idadi yao ni kubwa na inaongezeka kila siku.



    Nitoe shukrani zangu za dhati kwa mamlaka husika na serikali kwa ujumla kwa juhudi  na bidii zao katika kuhakikisha kivuko cha Ferry Kigamboni kinaboreshwa siku hadi siku.Nikiwa kama mkazi wa jiji hili ni shahidi tosha wa maendeleo ya kivuko hiki,nimekitumia tangu nikiwa darasa la kwanza mpaka sasa nimemaliza chuo.Matatizo mengi nimekuwa nikiyaona na kushuhudia hivyo najua maboresho kweli yamefanyika kwa kiasi fulani.Mfano mzuri ni ujio wa pantoni jipya la Mv Magogoni,pamoja na ujenzi wa ziada wa shushio au niite kama stand yetu ya basi,kwan kwa sisi wakazi hili pantoni ndio basi letu kwa shughuli za kila siku za kujenga taifa.Ninaomba na kuishahuri mamlaka na serikali kuwa huo uwe mwanzo wa mazuri katika jiji letu la kigamboni."Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Kigamboni", Amen


Moja ya Beach kongwe na nzuri iitwayo Mikadi. 
Navy Beach   ilyopo mkabala na maeneo ya Bandari kuu ya Dar-es-salaam.


Upepo na mazingira bora  ndio sababu tosha ya vijana kupenda eneo hili kwa mazoezi.

No comments:

Post a Comment